Katika taarifa iliyosomwa kwenye televisheni ya taifa, mamlaka nchini humo imesema kuwa kifo cha kiongozi huyo kilichotokea siku ya Jumapili kimethibitishwa baada ya operesheni hiyo kukamilika, lakini taarifa hiyo haikutoa maelezo zaidi.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilitangaza kitita cha hadi dola milioni tano kwa watakaotoa taarifa zitakazofanikisha kupatikana kwa Huzeifa, ambaye alishutumiwa kushiriki katika shambulio la mwaka 2017 nchini Niger lililowauwa wanajeshi wanne wa Marekani na wengine wanne wa Niger.
Kwa zaidi ya kipindi cha muongo mmoja uliopita, mashambulizi yanayohusishwa na makundi yenye itikadi kali ya al-Qaida na Dola la Kiislamu Afrika Magharibi (AQIM) yamesababisha vifo vya maelfu ya watu nchini Mali, Niger, na Burkina Faso na kusababisha hali ya usalama eneo la Sahel kuzorota.