Wizara ya mambo ya ndani ya utawala mpya wa kijeshi nchini Niger imepiga marufuku maandamano yote ya umma baada ya wafuasi wa mapinduzi hayo kuchoma moto makao makuu ya chama cha rais aliyepinduliwa.
Polisi walirusha vitoa machozi kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wameenda katika makao makuu ya chama cha PNDS Tarraya, ambako watu pia walikuwa wakirusha mawe na kuchoma magari.
“Maandamano ya hadhara kwa nia yoyote kwa vyovyote vile yanasalia kuwa marufuku hadi ilani nyingine. Serikali itahakikisha kwamba sheria inatekelezwa,” ilisoma taarifa ya wizara ya mambo ya ndani.
“Vitendo hivi, ambavyo vilifanywa na watu wasiofuata sheria, ambao wamefanya uharibifu na uovu na havitavumiliwa,” iliongeza taarifa hiyo.
Serikali itahakikisha kwamba sheria inatekelezwa,” ilisema taarifa ya wizara ya mambo ya ndani.
“Vitendo hivi, vilivyofanywa na watu wasioheshimu utawala wa sheria, vinajumuisha vitendo vya uharibifu na uovu na havitavumiliwa,” iliongeza.
Wizara hiyo imevitaka vyombo vya usalama kulinda raia na mali zao.