Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Stergomena Tax amesema jeshi sio sehemu ya siasa hivyo migogoro ya ardhi inayohusisha maeneo ya kijeshi yanapaswa kutatuliwa kwa ushauriano kwa kufuata sheria na taratibu zilizopo.
Dkt. Tax amesema hayo wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara ya Ulinzi na jeshi la kujenga Taifa kwa Mwaka wa fedha 2024/25 ambapo amesema maeneo ya Jeshi ni maalum kwa shughuli za Kijeshi ikiwemo Ulinzi wa Taifa.
“Maeneo yaliyotengwa kwaajili ya jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania hutengwa mahsusi kwa maslahi mapana ya taifa letiu hususani ulinzi wa Taifa letu niwaombe viongozi na wananchi wote kutoa ushirikiano kwa kuyalinda,kutoyavamia na kupelekea migogoro isiyo ya lazima na migogoro inapojitokeza inatakiwa itatuliwe kwa mashauriano na kufuata sheria na taratibu zilizowekwa na si kisiasa, Jeshi si sehemu ya siasa ni taasisi mahususi kwa kazi mahususi” Dkt. Tax