Waziri wa nchi ofisi ya Rais-TAMISEMI Suleiman Jaffo leo January 4, 2018 amefanya ziara kwa ajili ya kukagua changamoto zinazowakabili wakazi wa eneo la Buguruni kwa Mnyamani, ambapo amekuta barabara mbovu na hospitali ya eneo hilo zikiwa ni kero kubwa kwa wananchi.
“Ziara hii nimefanya ili kukagua changamoto zinazowakabili wananchi katika maeneo haya, kipaumbele changu kilikuwa maeneo mawili, katika barabara na kituo cha afya, nimeona matatizo yaliyopo hasa katika barabara, nimetoa maelekezo mpaka jumatatu viongozi wawe wamekaa kikao,” – Waziri Jaffo
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI YA JANUARY 4 2018? UNAWEZA KUYATAZAMA HAPA CHINI