Leo March 5, 2018 Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Vicent Mashinji ameongozana na Viongozi wengine Wakuu wa chama hicho katika kituo cha Polisi baada ya kutakiwa kuripoti kwa mara nyingine leo.
Akizungumza baada ya kutoka Polisi Dr. Mashinji amesema amehojiwa na kuachiwa kwa dhamana, kwa tuhuma za kusababisha mkusanyiko isivyo halali.
“Nimehojiwa kwa makosa ya kufanya mikusanyiko isiyo halali wakati tulikuwa katika kipindi cha uchaguzi, nimejaribu kuelezea matukio yote ya siku hiyo yaliyotokea, walitaka kujua kwa nini tulifanya maandamano,” -Dr. Vicent Mashinji
KCMC WAZUNGUMZIA UGONJWA WA MBOWE NA KULAZWA, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA
TAARIFA RASMI YA CHADEMA KUHUSU KULAZWA KWA MBOWE, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA