Kamanda wa kanda maalum ya Polisi DSM Lazaro Mambosasa amezungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali ikwemo suala la kifo cha mwanafunzi Akwilina Akwilini ambae aliuawa wakati wafuasi wa CHADEMA wakielekea kudai viapo vya wasimamizi wa uchaguzi kwa Mkurugenzi
Kamanda Mambosasa amesema bado upelelezi unaendelea kwa sababu silaha moja iliyomuua Akwilina bado haijajulikana na upelelezi unaendelea.
“Suala la upelelezi bado linaendelea, yapo maelekezo yaliyotolewa ambayo tunaendelea kufuatilia ili kuja kubaini, ikumbukwe silaha moja ambayo haijajulikana ni ipi ndio ilikwenda ikamgusa Akwilina lakini wale walikuwa ni wengi na kulikuwa hakuna ushahidi ni yupi alietenda hivyo” -Mambosasa