Leo January 31, 2018 Rais John Magufuli amezindua rasmi Hati ya Kusafiria ya Kielektroniki mjini Dar es salaam na kueleza kuwa hati hiyo ina alama nyingi za usalama hivyo itasaidia kupunguza kama si kuondoa kabisa uwezekano wa kughushiwa kwani taarifa zake zitakuwa zikipatikana kwenye mifumo ya kielektroniki tu.
Ameeleza pia kuwa hati hii mpya ya kusafiria itapunguza gharama na uwezekano wa kupotea pindi inaposafirishwa kwenda nje ya nchi nyingine kwa ajili ya kuomba visa huku ikiokoa muda wa kufanya mchakato mzima.
Rais Magufuli amesema kuwa hati hii ni mwanzo wa utekelezaji wa mradi mkubwa wa uhamiaji mtandao yaani e-migration, ambao umepangwa kutekelezwa kwa awamu nne. Awamu ya pili itahusu kufunga mfumo wa visa yaani e-visa pamoja na hati za ukaaji wakati awamu ya tatu itakuwa ya usimamizi wa mipaka kwa njia ya kielektronic yaani e-boarder management system.
Awamu ya nne itahusu kupanua huduma za uhamiaji mtandao kwenye ofisi za balozi nchini pamoja na Wilaya zenye shughuli nyingi za uhamiaji. Gharama za mradi huu ni Dola za Marekani Mil 57.82 sawa na Tsh Bilioni 127.2.
Mnigeria aliyekamatwa na Dawa za Kulevya Airport DAR