Kutoka nchini Kenya, katika Jimbo la Kajiando, wanafamilia nane wamefikishwa mahakamani wakishtakiwa kuhusika na kifo cha mke wa mtoto wao ambaye alikuwa mjamzito.
Inaelezwa kuwa wanafamilia hao walimnyonga hadi kufa binti huyo Priscillah Wanjiku wiki moja iliyopita akiwa nyumbani kwao.
Kwa mujibu wa Didmus Ndege, ambaye ni mwanasheria wa familia ya marehemu, mwili wa Priscillah uligunduliwa akiwa amefariki nyumbani kwa wakwe zake siku ya Jumapili alasiri.
“Alikuwa anaishi na mama yake huko Dandora lakini ilipofika weekend wakwe zake hao walimwita na kumwomba aende akawasaidie kazi za ndani kwasababu walikuwa wanatarajia wageni.” – Didmus Ndege
Bwana Ndege anaeleza kuwa baada ya ndugu wa binti huyo kuona kimya na amepotea kwa muda mrefu walipiga simu kwa wakwe zake na kumuulizia. Familia hiyo awali wakasema alikwenda kanisani na baadaye kudai aliingia chumbani kulala.
“Baada ya kwenda ya kufunga safari na kwenda kuangalia chumbani humo tuligundua ameshafariki tena akiwa amenyongwa ila akiwa amelala kitandani, hatukukuta kamba iliyomnyonga, jambo lililotupa utata kuwa inawezekanaje ajinyonge na tusikute kamba, na zaidi tukute amelala kitandani.” – Didmus Ndege
Alichokibaini Naibu Waziri Mavunde katika ziara ya kushtukiza Mwanza
“Hukumu ya Sugu tuliijua siku nyingi na imepangwa Hotelini” -Mbowe