Rais Mstaafu wa Zimbabwe Robert Mugabe amezungumza na vyombo vya habari jana March 16, 2018 ameeleza jinsi gani alisikitishwa na usaliti aliofanyiwa na Rais wa sasa wa nchi hiyo Emmerson Mnangagwa.
Mugabe ambaye alishinikizwa na jeshi la nchi hiyo kujiuzulu November 2018, ameeleza kuwa Rais Mnangagwa ndiye aliyehusika kwa kushirikiana na jeshi kumlazimisha kujiuzulu jambo ambalo ameliita ni Mapinduzi ya Kijeshi.
Mugabe ambaye ana umri wa miaka 94, aliliongoza taifa hilo la Zimbabwe tangu mwaka 1980 hadi alipolazimishwa kujiuzulu mwaka jana.
“Sikuwahi kufikiri kuwa mtu niliyemlea na aliyeletwa kwenye serikali na ambaye nilitetea maisha yake kwa bidii akiwa jela akikabiliwa na kunyongwa, kwamba kuna siku atanisaliti.” – Robert Mugabe
‘NABII ANAEGAWA HELA SHILLAH’ AZUNGUMZA KANISA KUFUTIWA USAJILI, KUITWA DODOMA
Mwalimu wa Mtoto Jasiri aliemshtaki Baba yake Polisi kwa kuuza shamba, kaongea