Mbunge wa Jimbo la Ubungo Saed Kubenea ametoa malalamiko yake kuhusu uchaguzi katika Jimbo la Kinondoni ambapo ametaja baadhi ya kasoro alizoziona katika uchaguzi huu ambao umefanyika leo February 17, 2018.
“Uchaguzi huu umevurugwa kwa kiwango kikubwa sana, Msimamizi amechelewa kutoa viapo kwa Mawakala, ameweka sababu za Vitambulisho ambazo hazipo katika sheria, kura zimepigwa kabala ya muda, Mawakala wetu wametolewa nje,” -Kubenea