Leo May 17, 2018 Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Simon Sirro amefanya uteuzi na mabadiliko kwa baadhi ya Makamanda wa polisi wa mikoa katika Mikoa mbalimbali Tanzania Bara na Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa jeshi la polisi nchini Barnabas Mwakalukwa imesema IGP Sirro amemteua Naibu Kamishna wa Polisi Maulid Mabakila aliyekuwa kuwa Mkuu wa Kitengo cha kuzuia uhalifu Makao makuu ya Polisi DSM kuwa Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Zanzibar.
IGP Sirro pia amefanya mabadiliko kwa Makamanda wa Mikoa ambapo Naibu DCI Zanzibar Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ramadhan Ng’anzi ameteuliwa kuwa RPC wa Arusha huku RPC Arusha Charles Mkumbo akihamishiwa Makao Makuu.
Pia aliyekuwa Kamanda wa polisi mkoa wa Mjini Magharibi Hassan Nassir Ali amehamishiwa Kaskazini Pemba na nafsi yake ikichukuliwa na Kamishna na msaidizi Thobias Sedoyeka.
Kamanda Hassan Nassir Ali alizishika headlines za vyombo vya habari Tanzania Baada ya kusambaa kwa video aliyokuwa anazungumzia suala la kuwa kamata na kuwafikisha mahakamani wanaume wanao jikoolesha au hata kuwasumbua wanawake wenye maumbile makubwa haswa sehemu za nyuma