Serikali imewaagiza Wakala wa Udhibiti wa Viwango (TBS), Wakala wa Vipimo (WMA) na Tume ya Ushindani (FCC) kufanya mapitio ya kanuni ili kupunguza viwango vya tozo kwa wenye viwanda na wafanyabiashara na kutoa marekebisho kabla ya Juni 30, 2019.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Joseph Kakunda amewaambia Waandishi wa Habari kuwa; Nakiri mbele ya Watanzania kuna malalamiko kuhusu kanuni zetu zinatoza matozo makubwa na kusababisha gharama za ufanyaji wa biashara na uendeshaji wa viwanda.
“Hivyo nimewaagiza TBS, WMA, FCC kufanya mapitio ya Kanuni ili kupunguza viwango vya tozo kwa wafanyabiashara na viwanda, pia nawaagiza kuongeza mapambano dhidi ya maofisa wala rushwa lengo likiwa kuongeza utendaji kazi,“amesema.