Wanasayansi wamegundua kuwa unywaji wa kahawa unasaidia mzunguko wa haraka wa damu kwa kusafisha calcium katika mishipa.
Taarifa iliyotolewa na “The Telegraph”, imesema wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Brazil cha Sao Paulo wamechunguza mpango wa lishe na kiwango cha calcium kwenye mishipa ya wafanyabiashara karibu 4,400 wa kahawa.
Kwa mujibu wa habari hiyo, utafiti huo umeonyesha kuwa wanywaji wa kahawa wana kiwango kidogo cha calcium katika mishipa yao na mzunguko mzuri wa damu.
Hata hivyo wanasayansi wameonya kuwa ni vizuri kutozidisha vikombe vitatu vya kahawa kwa siku.
Utafiti huo umechapishwa katika jarida la “American Heart Association”.