Teknolojia ya usafirishaji ya Uber inaendelea kusambaa nchi mbalimbali duniani ambapo kampuni hiyo imejipanga kuzindua huduma mpya ya kusambaza chakula Afrika Mashariki ikianza na jiji la Nairobi nchini Kenya kabla ya mwaka 2018 kuisha.
Huduma hiyo inayojulikana kama Uber Eats kwasasa inafanya kazi katika miji 200 duniani kote na ikishirikiana na migahawa 80,000.
Kwa mujibu wa Msemaji Mkuu wa Uber Afrika Mashariki Janet Kemboi ambaye hajataja lini haswa huduma hiyo itazinduliwa, ameeleza kuwa bado wanafanya mazungumzo na migahawa mbalimbali kuingia mkataba na Uber ili biashara hiyo ianze.
BREAKING: Timotheo Wandiba ahukumiwa Miaka 81 jela