Waziri wa kilimo Dr. Charles Tizeba amefanya ziara mkoani Kagera ambapo amekumbana na changamoto kubwa ikiwemo biashara ya magendo ya kahawa inayouzwa nchini Uganda pamoja na kuuza kahawa ikiwa bado ipo shambani maarufu kama “Butula”.
Dr. Tizeba amesema kuwa kuna Viongozi wakubwa kabisa ndio vinara wa biashara ya butula na kuna wengine wanashiriki kuvusha kahawa kwenda Uganda na wanajulikana na tayari kuna fedha karibia Bilioni 9 zishatawanywa wilayani Kyerwa kwa ajili ya biashara hiyo.
“Mtu wa Mkuranga Unadanganywa kwa 200 unakubali” -Dr. Mwanjelwa