Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma wa CUF kwa upande wa Maalim Seif, Mbarala Maharagande amefunguka na kuweka wazi kuwa Profesa Lipumba pamoja amepanga njama kuwafukuza madiwani wote wa CUF katika mkoa wa DSM.
“Lipumba amepanga njama za kutaka kuwafukuza uanachama madiwani kwa tiketi ya CUF DSM, wakiwemo Manaibu Meya, kutokana na madiwani hao kukataa kumsaidia Lipumba katika kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Kinondoni.”-Maharagande
“Lipumba na watu wake wamejikuta katika wakati mgumu kwa uamuzi wao wa kusimamisha mgombea wakipingana na uamuzi wa UKAWA wa kusimamisha mgombea mmoja kutoka miongoni mwa vyama washirika”- Maharagande.
“Uamuzi huo wa Lipumba ambao umetafsiriwa kuwa ni mpango wa kutaka kuzigawa kura ili kuisadia CCM ishinde, umeshitukiwa na wananchi wa jimbo la Kinondoni na kusababisha kususiwa mikutano yao ya kampeni na wadau mbalimbali”– Maharagande
“Tunawatia watu umasikini, hii sio haki” –Hussein Bashe