“Nina hela kuliko serikali” ni kauli aliyoinukuu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Edward Kichere kutoka kwa Askofu Kakobe. Kauli hiyo imeifanya TRA kuanzisha uchunguzi dhidi yake.
“Tunaambiwa serikali imezidiwa pesa na Askofu Kakobe, baada ya kauli ya Kakobe ilibidi tupitie kumbukumbu zetu tuone jinsi Kakobe anavyolipa kodi, utajiri unaendana na ulipaji kodi, hatuna kumbukumbu za ulipaji kodi wake,” – Kamishina Kichere
“Sisi watu wa kodi tunataka tujiridhishe kuhusu suala la kodi linalomhusu Askofu kakobe, sisi ni watalaamu wa kodi basi tuna uhakika tutafahamu kama kipato anachosema kinapatikana na sadaka tu au kuna shughuli nyingine anazozifanya,” – Kamishina Kichere
AGIZO LA WAZIRI NCHEMBA KAMA HUNA KITAMBULISHO CHA UTAIFA, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA