Leo April 18, 2018 kutoka Zanzibar ninayo stori inayomhusu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha ambaye amemaliza muda wake wa majukumu ya tume hiyo kwa kipindi cha miaka mitano ambapo yeye na wajumbe wa tume hiyo wamekabidhi ripoti yao ya kazi.
“Ndani ya miaka mitano tume imeweza kuendesha jumla ya chaguzi ndogo nne, zikiwemo chaguzi ndogo tatu za Udiwani na chaguzi moja ya uwakilishi pamoja na kusimamia uchaguzi Mkuu wa October 25, 2015 na ule wa marudio yake March 20, 2016.” -Jecha
“Tume imefanya mapitio ya majimbo ya uchaguzi na kubadilisha mipaka ya majimbo ya uchaguzi, majina ya majimbo na kuongeza idadi ya majimbo kutoka 50 hadi 54” –Jecha
Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein ameipongeza Tume hiyo kwa kutekeleza vyema majukumu yake ndani ya miaka mitano kwa kuendesha chaguzi zote .
“Tume hii inastahiki pongezi kwa kuifanikisha vyema kazi waliyopewa ikiwa ni pamoja na kuendesha chaguzi zote ukiwemo uchaguzi Mkuu, chaguzi ndogo na ule uchaguzi wa marudio ambazo zote hizo zilifanywa kwa ufanisi mkubwa” Jecha-
Wajumbe waliomaliza muda wao ni Mwenyekiti mwenyewe Jecha Salim Jecha, Jaji Abdul-hakim Ameir Issa, Balozi Omar Ramadhan Mapuri, Nassor Khamis Mohammed, Ayoub Bakari Hamad, Haji Ramadhan Haji na Salmin Senga Salmin.