Leo June 27, 2018 nakusogezea taarifa kuhusu ujio wa Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangangwa ambaye anatarajiwa kuwasili nchini kesho kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
Hii ni ziara ya kwanza kwa Rais Mnangangwa kuja nchini tangu aingie madarakani mwezi November mwaka jana.
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inasema lengo la ziara hiyo ni kujitambulisha kwa Rais John Magufuli na wananchi wa Tanzania.
Rais Mnangangwa atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais John Magufuli na pia kutembelea chuo cha sanaa cha Kaole Bagamoyo ambacho awali kilitumika kutoa mafunzo kwa wapigania uhuru kutoka nchi za Kusini mwa bara la Afrika na yeye akiwa ni mmoja wapo aliyepata mafunzo katika chuo hicho.
King Majuto “Zipo Kampuni nimefanya kazi, mikataba ninayo wamekimbia na hela zangu”