Kampuni ya ”The Network” kupitia mchezo wake nambari moja nchini Tanzania wa Tatu Mzuka Leo November 1 2018 wamezindua kampeni mpya inayoitwa ”mamilionea 100 kwa siku moja” ambapo takribani Watanzania 100 watakuwa mamilionea mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka huu.
Kampuni ya Tatu Mzuka imeamua kuzindua kampeni hii baada ya kupokea maombi mbalimbali kutoka kwa wachezaji wake kupitia kurasa za mitandao ya kijamii wakitaka kuona kampuni hiyo ikitengeneza mamilionea wengi zaidi.
Hiyo yote imekuja siku chache baada ya kutangaza wiki iliyopita kwamba imetoa zaidi ya shilingi milioni 340 ndani ya siku nne huku washindi wawili kushinda milioni 260 na milioni 60 kupitia SupaMzuka Jackpot.
Kampeni hii itaanza rasmi siku ya Jumapili ya Novemba 4 2018 na kila Jumatano na Jumapili watatangaza washindi kumi walioingia kwenye kinyang’anyiro cha fainali ya ”mamilionea 100 ndani ya siku 1”