Baada ya kutolewa na Madagascar katika hatu ya 16 bora ya AFCON 2019 kwa mikwaju ya penati 4-2 baada ya dakika 120 kumalizika kwa sare ya 2-2, kocha mkuu wa Congo Frorent Ibenge amefunguka na kueleza masikitiko yake kuhusu muamuzi wa mchezo huo.
Ibenge ameeleza kuwa amesikitishwa zaidi kutokana na kuwa anamfahamu vizuri muamuzi aliyechezesha mechi na kuujua vizuri uwezo wake ila amesikitishwa na kuona akichezesha kwa kutokuata haki na badala yake amekuwa akiipendelea Madagascar.
“Tuna huzuni kwa sababu tumepoteza unapokuja kucheza unataka kushinda ila leo tumepoteza hivyo tuna huzuni tunarudi nyumbani na hongera kwa Madagascar, nakuacha wewe utoe comment hiyo kuhusu muamuzi ila imetuhuzunisha kwa hilo, kwa sababu muamuzi alikuwa na uwezo wa kuchezesha vizuri zaidi kuliko alivyochezesha leo kwa sababu namjua na huwa yupo bora kuliko alivyokuwa leo”>>>Ibenge
VIDEO: Kinachomfanya Bongo Zozo asite kuomba uraia wa TZ, Maisha yake?