Naibu Spika Dr Tulia Ackson amefanya ziara katika maeneo mbalimbali mkoani Mbeya ikiwemo Shule ya Msingi Iyela ambapo ametoa msaada wa mabati 100 kupitia taasisi yake ya TULIA TRUST pamoja na mifuko 250 ya cement kutoka kwa mfadhili kutoka falme za kiarabu Sheikh Khalid Bucheri ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Naibu Spika.
Dr Tulia pia ameahidi kutatua changamoto nyingine alizopewa ikiwemo maji, barabara na afya ambapo amesema…>>>“Niwashukuru na kuwapongeza wananchi wote kwa juhudi mlizozianza kwa ujenzi wa madarasa manne, hili sio jambo la mchezo hata kidogo. Wananchi mmeamua kujiletea maendeleo wenyewe kwa kushirikiana na viongozi wenu”
“Nimeambiwa kwamba mna changamoto nyingi ikiwemo miundombinu ya maji, hili nimelipokea na nitalifikisha katika Wizara husika. Kwenye hili la kituo cha afya niahidi kama TULIA TRUST kwamba tutashiriki katika ujenzi wa kituo hadi pale tutapofikia ili kusaidia wananchi wetu” –Dr Tulia