Mamlaka ya Jimbo la Lagos nchini Nigeria imesema itaanza mara moja kutekeleza marufuku ya matumizi ya bidhaa za plastiki.
Kwa mujibu wa Kamishna wa mazingira wa Lagos Tokunbo Wahab plastiki zisizoharibika ni tatizo kubwa la uchafuzi wa mazingira, na zinaziba mifereji ya maji.
Maafisa wa serikali wanasema watatumia sheria ya mwaka wa 2009 kuwatoza faini au kuwafunga jela watakaokiuka agizo hilo.
Lagos ni mojawapo ya miji yenye watu wengi zaidi barani Afrika.
Wataalamu wa kimataifa wanakadiria kuwa Nigeria inazalisha tani milioni 2.5 za taka za plastiki kila mwaka.
Hatua sawa na hii imechukuliwa na nchi ya Kenya ikiwa ni hatua ya kukabiliana na uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na matumizi ya bidhaa za plastiki.