Gavana wa jimbo la kaskazini-mashariki la Adamawa nchini Nigeria ametangaza amri ya kutotoka nje kwa saa 24 kufuatia uporaji wa maduka ya vyakula na maghala katika mji mkuu wa jimbo hilo, Yola.
Mamia ya watu walinaswa kwenye video, wakivunja maghala, wakibeba magunia ya nafaka na vitu vingine vya nyumbani.
Kwa amri ya Gavana Ahmadu Umaru Fintiri, maafisa wa usalama wametumwa kutekeleza amri ya kutotoka nje.
Mwezi uliopita, Nigeria ilimaliza utaratibu wa kutoa ruzuku ya mafuta, na kusababisha kupanda kwa bei ya vyakula na petroli.
Hii ilifuatia uporaji mkubwa wa maduka ya vyakula katika mji mkuu wa jimbo, Yola.
Msemaji wa Umaru Fintiri alisema gavana wa jimbo la kaskazini-mashariki mwa Nigeria alitangaza amri ya kutotoka nje “kutokana na kuongezeka kwa ghasia za makundi ya watu wanaoshambulia watu na biashara.”
Msemaji wa polisi alisema kuwa maafisa walikuwa wametumwa kutekeleza agizo la kukaa nyumbani kwa mtu yeyote ambaye sio kwa kile kinachozingatiwa kuwa majukumu muhimu.
Janga la uviko 19 na changamoto zengine zimetajwa kuchangia katika kudorora kwa hali ya uchumi nchini Nigeria.