Leo February 28, 2018 Stori zinazohusu Madiwani kuhamia Chama cha Mapinduzi zinaendelea kushika headlines ambapo Madiwani wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamejiuzulu nafasi zao na kuhamia CCM kwa madai ya kumuunga mkono Rais Magufuli katika utendaji wake wa kazi.
Madiwani hao ni Joseph Mongita aliyekuwa Diwani wa kata ya Machila pamoja na Mikael Macheba Kunani aliyekuwa Diwani wa kata ya Ikoma.
Wakizungunza baada ya kujiuzulu wamesema kwa kipindi chote walipokuwa Viongozi walikuwa wakitekeleza ilani ya CCM.
FULL VIDEO: SUGU NA MASONGA WAKIPELEKWA GEREZANI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA