February 15, 2018 Mahakama ya Hakimu mkazi Mkoa wa Dodoma imemuachia huru aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Sadifa Juma Khamis baada ya upande wa Jamhuri kuwasilisha maombi ya kuifuta kesi ya rushwa iliyokuwa ikimkabili.
Uamuzi huo umetolewa mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Emmanuel Fovo baada kuridhia ombi la wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Biswalo Biswalo kufuatia kuiomba Mahakama kuifuta kesi hiyo.
Ikumbukwe kwamba December 9, 2017 Sadifa alikamatwa na TAKUKURU akiwa nyumbani kwake Dodoma na kutuhumiwa kutoa rushwa kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa umoja huo wakati wa kampeni za kumpata Mwenyekiti mpya wa umoja huo.
Ayo TV na millardayo.com imempata kwenye Exclusive Interview aliyekuwa Wakili wake katika kesi hiyo Godfrey Wasonga ambaye hapa anaelezea mwanzo mwisho..
LIVE: Mtoto wa Miaka 2 amerudishwa nchini, Baada ya wazazi wake kukamatwa na dawa za Kulevya China