Leo February 14, 2018 katika stori za Kimahakama niliyoipokea ni kuhusu Wazanzibari 40,000 kufungua kesi katika Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki (EACJ) kupinga uhalali wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Kesi hiyo ilifunguliwa February 13, 2018 katika Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki (EACJ) na Rashid Salum Adiy kwa niaba ya wenzake 39,999, katika Masijala ndogo ya mahakama hiyo iliyoko jijini Dar es Salaam.
Wadaiwa katika kesi hiyo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
BREAKING: Kamanda Kinondoni Kuhusu Mwili Uliokotwa Coco Beach