Imepita miezi miwili sasa tangu wafuasi wa dini ya Kikristo katika nchi mbalimbali duniani kusherehekea Krismasi.
Hata hivyo nchini Columbia katika kijiji cha Quinamayó ndio wanasherekea Krismasi kipindi hiki na wametengeneza sanamu ya mtoto Yesu mweusi.
Inaelezwa kuwa utamaduni huu ulianza tangu enzi za utumwa wakati mababu zao walipozuiwa kusherehekea Krismasi tarehe 24 December na hivyo wakachagua mwezi February kila mwaka kufanya sherehe hizo.
Kama sehemu ya sherehe hizi, wanakijiji hutembelea nyumba mbali mbali wakimtafuta ‘mtoto Yesu’, ambaye huwakilishwa na sanamu ya mbao ambayo hutunzwa na mmoja wa wanavijiji nyumbani kwake kwa kwa kipindi cha mwaka kilichosalia.
Pindi sanamu inapopatikana, hutembezwa kijijini kizima na wakazi wa rika zote waliovalia kama malaika na wanajeshi na sherehe zote huisha asubuhi.
SAFARI YA KWANZA YA RAIS MAGUFULI NJE YA TANZANIA 2018, UGANDA