Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi anaendelea na ziara zake za utatuzi wa migogoro ya ardhi nchini, ambayo imejikita zaidi katika kutatua migogoro ya ardhi ya mikoa ya kanda ya Magharibi, kaskazini na ile ya Kanda ya Ziwa hapa nchini.
Akiwa katika ziara hiyo katika mkoa wa Mara, Waziri Lukuvi amemuondoa Mpima Ardhi wa manispaa ya Musoma John Kapera na Kumtaka katibu tawala wa mkoa wa Mara amuondoe katika kituo chake cha kazi kuanzia leo December 21 2016
John Kapera amedaiwa kuwa anasababisha matatizo mengi katika manispaa hiyo na kupelekea kuwa kero kwa wananchi wa Musoma katika kupima ardhi na kumilikisha.
HEKAHEKA: Jamaa anaishi na mtoto wa dada yake na wamezaa watoto wawili, Bonyeza play hapa chini kusikiliza