Jumapili ya April 29 2018 mchezo wa watani wa jadi kati ya Simba na Yanga ulichezwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam na kuhudhuriwa na mashabiki mbalimbali, dakika 90 za mchezo huo zilimalizika kwa Simba kupata ushindi wa goli 1-0 lilifungwa na Erasto Nyoni dakika ya 38, mchezo huo ulikuwa na presha na matukio mbalimbali yalijitokeza.
Ukiachilia tukio la Hassan Kessy kuoneshwa kadi nyendu tukio lingine lililokuwa gumzo ni Kelvin Yondani kumtemea mate Asante Kwasi wa Simba kiasi cha kufanya mjadala kuwa mkubwa mtandaoni, mchezaji wa zamani wa Yanga Mrisho Ngassa yeye amelizungumzia hilo kupitia ukurasa wake wa instagram kuandika mtazamo tofauti.
“Waweza kujaji vitu vingi sana katika mpira wetu wa Hapa Tanzania mengi watu hawayaoni kutokana kila mtu anavutia upande wake kweli kitendo ambacho kafanya Yondani sio kizuri lakini angalia mechi ilikuwa yauzito kiasi Gani hayo katika mpira yapo haswa mpira wa ushindani kama wa jana”>>> Mrisho Ngassa
“Ukija kwa Okwi kampiga kipa ambaye kadaka mpira mfano angemvunja mguu lakini yote ile ni mbinu za kuogopwa uwanjani hivyo ndivyo na Simba kiliwapa ushindi mpaka kupata Goal kwani kipa kaisha gongwa kwenda anaogopa, mimi kikubwa hayo yamepita ya kutemeana mate kumpiga mtu mashabiki mnaongea huku lakini sisi wachezaji ukutana na kuombana radhi hivyo hongera Simba kwa ushindi pole Kwasi”>>> Mrisho Ngassa
VIDEO: Mapokezi ya Yanga Airport DSM na alichokisema kocha wao