Baada ya kuenea kwa taarifa za club ya Simba SC kudaiwa kumfukuza kazi kocha wao msaidizi Masoud Djuma, bila kutoa taarifa rasmi mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa club hiyo Haji Manara kutumia ukurasa wake wa instagram amekanusha taarifa hizo.
“Leo nimepigiwa simu nyingi toka kwa waandishi wa habari na washabiki wa Simba kutaka kujua ukweli wa taarifa zilizoandikwa kwenye gazeti moja likidai kocha msaidizi wa Simba anaondoka baada ya kutofautiana na kocha Mkuu Patrick Aussems”
“Kocha huyo Masoud Djuma inaarifiwa pia eti amekosana na baadhi ya wachezaji wetu, simu hizo zimeambatana na msg nyingi za WhatsApp na sms pamoja na kwenye page yangu ya Instagram”
“Hakuna niliyemjibu zaidi ya kuchukizwa na tabia ya baadhi ya watu kukubali kila porojo inayoandikwa ama kwenye baadhi ya magazeti au mitandaoni!! Ieleweke hakuna atakaekaa Simba milele sio Masoud au Aussems na hata mimi ninaeandika hii makala fupi”
“Lakini wote tutaondoka pale muda wetu utakapofika na kwa utaratibu maalum, Sasa huku kwenye michezo..bado kuna dhana potofu Mwandishi anaweza kuandika lolote na chochote anachojisikia bila kuulizwa wala kuchukuliwa hatua na ndio maana leo story za kupikwa zimekuwa nyingi kupita maelezo”
“Umezuka mtindo inapikwa story kisha ndio unaulizwa eti ili ubalance story!!🤣 Haji huwa hahangaiki na kubalance porojo na hekaya..Haji anashughulikia mambo ya msingi ya maendeleo ya Taasisi”
“Ukitaka kuamini hizo cooked stories zote hazina sources zinawekwa kusudi kwa dhamira zao..na hazibalance kwanza..zinaandikwa kisha ndio tunaulizwa!! Narudia tena na tena kabla ya kupika hizo porojo ni vema mkabalance kwanza kama taaluma inavyotaka”
“Kuliko kuandika kisha mwandishi wa gazeti hilo hilo anataka kubalance!! Na kwa mashabiki wetu sio kila kinachotoka migodini ni madini mengine ni michanga tu kama iliyopo ardhini”
“Walau ingekuwa Makanikia!! Nimalizie kwa kuwaambia Simba ni shwari na kilichoandikwa ni hekaya na hadithi sawa na zile za Abunuwasi..tusitolewe mchezoni kirahisi rahisi..tuendelee kuwa wamoja na tusiyumbishwe kwa maneno ya mahotelini”
Mkata Vimeo
De Le Boss
TFF imemfungia maisha mjumbe wa kamati ya Utendaji