Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars yenyewe imekosa nafasi ya kushiriki fainali za Kombe la dunia baada ya kutolewa mapema katika hatua za awali na timu ya taifa ya Algeria ambao na wenyewe wamekosa nafasi ya kushiriki fainali hizo.
Taarifa ikufikie kuwa pamoja na Tanzania kukosa nafasi ya kushiriki michuano hiyo lakini kuna mchezaji mwenye asili ya Tanzania atakayeiwakalisha Tanzania kwa kuichezea timu ya taifa ya Denmark Yusuf Yurary Poulsen ambaye pia anaichezea club ya RB Leipzig inayoshiriki Ligi Kuu Ujerumani Bundesliga.
Poulsen kwa sasa amejumuishwa katika kikosi cha awali cha timu ya taifa ya Denmark kitakachoshiriki Kombe la Dunia 2018, Poulsen ametajwa katika list ya wachezaji 35 ambapo kikosi hiko kitachujwa na kubakia wachezaji 23 kwa ajili ya World Cup na kuna uwezekano mkubwa Yussuf akajumuishwa katika kikosi cha wachezaji 23 kutokana na mchango wake aliouonesha wakati wa game za kufuzu.
Timu ya taifa ya Denmark yenyewe imepangwa Kundi C lenye timu za Ufaransa, Australia na Peru ambapo kundi hilo itakuwa ni nafasi kwa Poulsen kucheza dhidi ya wachezaji wakubwa kama Paul Pogba wa Man United na Antoinne Griezmann wa Atletico Madrid ambao wote watakuwa wanaitumikia Ufaransa.
Yusuf Poulsen baba yake ni mtanzania wa kuzaliwa wa Tanga, mzee Yurary ambaye alifariki kwa kansa wakati Yussuf akiwa na umri wa miaka 6, mama yake ni raia wa Denmark, Yussuf Poulsen wengi tumemfahamu hivi karibuni baada ya mafanikio yake Bundesliga lakini ana asili ya Tanzania.
AyoTV iliwahi kufanya exclusive interview na Yussuf Poulsen kuhusiana na maamuzi yake ya kuichezea Denmark na sio Tanzania
Haji Manara alivyokuja na takwimu leo mbele ya waandishi wa habari