Kesho Jumapili ya April 29 2018 uwanja wa Taifa Dar es Salaam utachezwa mchezo wa mzunguuko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Yanga ambao kwa sasa kila mmoja anajitihada za kuhakikisha wanatwaa Ubingwa wa Ligi hiyo na wakiamini ushindi katika mchezo dhidi yao ndio utatoa muelekeo wa Ubingwa.
Afisa habari wa Simba Haji Manara ameamua kuweka wazi maswali wanaouliza baadhi ya watu kutokana Simba na Yanga kutokea zote kwa pamoja zimeweka kambi mjini Morogoro, kitu ambacho hakijazoeleka, mara nyingi Simba hupenda kwenda Unguja wakati Yanga wao hupenda kwenda Pemba kuweka kambi mchezo dhidi yao ukikaribia.
“Imetokea tu kwa bahati mbaya wala haikuwa kitu maalum sisi tumeuchukulia huu mchezo kwa uzito mkubwa lakini kwa plan zile zile tu, mara kwanza tulitoka Njombe tukaweka kambi Morogoro, tulivyotoka tena Iringa kazima tuweke kambi Morogoro na wao kwa sababu wametoka Mbeya ndio maana wameweka kambi Morogoro”>>>Haji Manara
VIDEO: Mapokezi ya Yanga Airport DSM na alichokisema kocha wao