Shirikisho la soka Tanzania TFF leo limetangaza adhabu ya makamu wa Rais wa TFF Michael Richard Wambura anayetuhumiwa kwa makosa matatu, moja kupokea pesa za TFF isivyo halali, kugushi na kushusha hadhi ya TFF.
Baada ya kamati ya maadili ya TFF kukaa jana Jumatano ya March 14 2018, leo kamati ya maadili imefikikia maamuzi ya kumfungia maisha Michael Richard Wambura kujihusisha na soka baada ya kukutwa na hatia katika makosa yote matatu, amefungiwa maisha kujihusisha na soka.
Baada ya Wambura kufungiwa aliongea na waandishi wa habari kuhusiana na yeye kufikishwa kamati ya maadili.
TFF imetangaza adhabu kwa makamu wake wa Rais TFF