Leo Mei 24, 2019 Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF) Tanzania limebainisha kuwa vifo vya watoto wachanga na wajawazito ni miongoni mwa changamoto inayozikumba nchi nyingi duniani, ikiwemo Tanzania.
Mtaalamu wa Mawasiliano wa (UNICEF) Tanzania, Usiah Mkoma amesema moja kati ya mbinu inayoweza kutumika kuielimisha jamii ni kutumia vyombo vya habari hasa Wahariri.
Mkoma amesema wakina mama Wajawazito 8,200 hufa kila mwaka wakati wakijifungua na asilimia 50 ya watoto walio chini ya miaka 5 hufa pia kila mwaka ndani ya mwezi mmoja baada ya kuzaliwa kwa changamoto
mbalimbali.
“Muhimu ni kuhakikisha ndani ya siku 42 baada ya kujifungua, mama aendelee kuwa chini ya uangalizi wa wataalam wa afya ili waweze kukabiliana na changamoto zinazoweka kujitokeza kama vile kifafa cha mimba,’ amesema Nkoma.