Taarifa ambazo zimeripotiwa jioni ya November 8 2016 zimesema kuwa aliyewahi kuwa Waziri wa Elimu Tanzania, Joseph Mungai amefariki dunia huku taarifa za awali zikidai kuwa alianza kwa kutapika mfululizo, familia imedai kuwa tatizo hilo limemkuta baada ya kudaiwa kula kitu kibaya.
Taarifa za kifo zilizothibitishwa na mkuu wa kitengo cha mawasiliano ya umma Hospitali ya Muhimbili, Aminiel Bubwerwa Aligaesha amesema wamethibitisha kifo chake ila hakuwa amelazwa hospitalini hapo…………
>>> ‘hakuwa amelazwa hospitali ya Taifa Muhimbili, sisi tumepokea mwili wake, amekuja akiwa ameshakufa na sisi tumepokea mwili wake katika idara yetu ya magonjwa dharura na madaktari wetu wakathibitisha kifo chake na kupeleka mwili wake kwenye chumba cha kuhifadhi maiti’
KAMA HUKUPATA NAFASI YA KUPITIA HABARI ZA MAGAZETI YA TANZANIA NOV 8 2016, UNGANA NA ALICE TUPA WA AYO TV KWA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI