Leo May 18, 2018 Mlipuko mkubwa umetokea katika volkano ya Kilauea katika jimbo la Hawaii nchini Marekani na kuzua wasiwasi zaidi kwa wakazi wa eneo hilo.
Mlipuko huo ulirusha majivu futi 30,000 juu angani pia ulirusha juu mawe makubwa yanayodhaniwa uzito wake kuzidi kilo moja na baadhi inakadiriwa kuwa yanaweza kuwa na uzani wa tani.
Mlipuko huo umetokea saa kumi na robo alfajiri saa za Marekani. Wanasayansi wanasema bado kuna uwezekano mlipuko mwingine kutokea.
Watu waliokuwa wakifanya kazi katika kituo cha kufuatilia volkano hiyo waliokuwa kwenye mbuga ya taifa ambapo kunapatikana volkano hiyo wamehamishwa.