Leo June 22, 2018 nakusogezea stori kutoka huko nchini China ambapo unaambiwa kuwa baada ya Mahakama moja nchini Korea Kusini kuweka katazo la Wananchi wake kutokula nyama ya mbwa mambo ni tofauti huko nchini China ambapo unaambiwa kuwa Wananchi wa nchi hiyo wameanza kusherekea tamasha la kila mwaka la ulaji wa nyama ya mbwa.
Tamasha hilo la kila mwaka lililozinduliwa June 21 mwaka huu linajulikana kama Tamasha la Yulin ambapo Watu hujivinjari kwenye migahawa na masokoni na kula nyama ya mbwa kwa wingi.
Aidha tamasha hilo ambalo limeanzishwa mwaka 2009 lilisemekana kutofanyika mwaka huu kwa kile kilichodaiwa kuwa mamlaka italizuia lakini mambo hayakuwa hivyo ijapokuwa hakuna shamra shamra katika tamasha hilo kama ya miaka iliyopita.
Taifa la China linatajwa kuwa kati ya mataifa ambayo Wanachi wake wanakula nyama ya mbwa kwa wingi duniani ingawa baadhi ya Wanaharakati wanapinga ulaji huo wa nyama ya mbwa kwa kile wanachokidai kuwa mbwa ni rafiki wa binadamu hivyo hastahili kugeuzwa kitoweo.