Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brig. Gen. Emmanuel Maganga amewaonya wananchi Wilayani Kibondo kuacha kuwaingiza nchi kinyemela vibarua kutoka nchi jirani ya Burundi badala yake wafuate utaratibu wa kuomba vibali maalum kutoka kwa Watendaji wa Vijiji, Kata na Wakuu wa Wilaya ili vibarua hao wajulikane na kufanya kazi kwa utaratibu.
Maganga amesema Serikali Mkoani Kigoma imeshaanza kutengeneza utaratibu wa kutoa vibali maalum kwa Vibarua hao kutoka nchi jirani ya Burundi ili waweze kuingia na kufanya kazi za vibarua katika Vijiji na Wilaya zinazopakana na Burundi.