Mitandao ya kijamii ni sehemu nyingine ambayo inayofikisha ujumbe kwa urahisi zaidi, ni sehemu ambayo ukiweka chochote ndani ya dakika 10 kinakua kimesambaa sehemu mbalimbali za dunia kutokana na watu wengi kujiunga na mitandao mbalimbali.
Mmoja wa Wakazi wa Mwanza alimtumia Mwanadada Mange Kimambi video fupi ikionyesha Kiwanda ambacho bomba lake linatoa moshi na akasikika akiongea kwenye hiyo video “huo moshi unaoonekana hapo kuna kiwanda kinaitwa Nyakato Steel kinachafua hali ya hewa ni hatari, Wananchi wa Igoma afya zinaumiza huku”
Baada ya kupost video hiyo Mange aliandika watu wamtag Waziri January Makamba ambae ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anaeshughulikia Muungano na Mazingira ili ajionee malalamiko hayo.
Dakika kadhaa baadae Waziri January Makamba alijibu kwenye hiyo post kwa kuandika kuwajulisha wote waliolalamika kwa kuandika >>> “jmakamba @mangekimambi_ nimeona. Tutatuma watu. Asante“
January Makamba ni miongoni mwa viongozi wa Tanzania ambao hujibu sana maoni au comment za Wananchi kwenye mitandao ya kijamii na kufanya iwe rahisi kwa watu wenye madukuduku yao kuyafikisha au kusikilizwa kwa urahisi zaidi kuliko kutumia mifumo mingine ambayo ni ngumu kumfikia.
Miongoni mwa Viongozi wengine ambao hutumia mitandao yao binafsi kuweka kazi wanazofanya au kujibu comments au post za Wananchi ni pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii Dr. Kigwangalla, Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe, Waziri wa Uchukuzi Profesa Mbarawa, RC wa Dar es salaam Paul Makonda, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu n.k
ULIPITWA? Nape apingana na mapendekezo ya Serikali… bonyeza play hapa chini kumtazama
AGIZO LA JPM KUHUSU MWANAMKE ALIEANGUA KILO MBELE YAKE… BONYEZA PLAY HAPA CHINI
UNAZITAKA BREAKING NEWS FASTAFASTA? Jiunge na Reporter wako Millard Ayo kwa kubonyeza kifuatacho SUBSCRIBE >>> YOUTUBE , APP YA MILLARD AYO, FACEBOOK , INSTAGRAM