Kumekuwa na malalamiko kwa watumiaji wengi wa simu za mkononi kutokana na kukatwa gharama za huduma ambazo hawajaziomba, ikiwemo kuunganishiwa miito ya simu na nyinginezo.
Kama hukupata nafasi ya kusikiliza Bunge jana Novemba 25, ilihojiwa kuhusiana na suala hilo ambapo Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia alitolea majibu pamoja na suala la baadhi ya maeneo kuwa na matatizo ya mtandao.
“… Katika makubaliano kati ya Serikali na kampuni mpya ya simu ya Viatel, ambayo imekubali kujenga minara na kupeleka mawasiliano katika maeneo yote ambayo hayana mawasailiano nchini, tumewapa orodha ya Vijiji elfu nne ambavyo havina mawasiliano kote Nchini au vina mawasiliano ni hafifu, na tumekubaliana tumewekeana mkataba kwamba maeneo yote hayo ikiwemo maeneo ya jimbo na Nyag’wale yatapata mawasiliano kabla ya mwezi Novemba mwaka huu…“– January Makamba.
“... Kuhusu miito ambayo inaingiziwa kwa wateja bila ridhaa yao, Serikali inatambua kwamba hili ni tatizo na sisi kama Wizara tumewaandikia barua na tumezungumza na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ambayo ina wajibu wa kusimamia jambo hili kuhakikisha kwamba halifanyiki lakini na maslahi ya watumiaji wa simu yanalindwa, kwa hiyo tutaendelea kulifuatilia kuhakikisha kwamba Sheria inazingatiwa ili watumiaji wasidhulumiwe…”– January Makamba.
Kumsikiliza Naibu Waziri huyo wakati akijibu maswali hayo, bonyeza play hapa.
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook