Maadhimisho ya Wiki ya Wanawake Duniani inaendelea na mengi yanazungumzwa nchini, kuhusiana na changamoto zinazokabili wanawake, fursa zilizopo kwa ajili yao na ustawi wao kwa ujumla.
Ripoti ya hivi karibuni ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya (WHO) inaonesha kuwa wanawake milioni 195 duniani kote wanaathiriwa na magonjwa ya figo na 600,000 kati yao hupoteza maisha kila mwaka.
Inaelezwa kuwa magonjwa ya figo yanashika nafasi ya 8 kama chanzo cha vifo vya wanawake na kwamba wanawake wako hatarini zaidi kupata mgonjwa haya ya figo ukilinganisha na wanaume.
Akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani March 8, 2018, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndugulile ameeleza kuwa matatizo ya figo yanaendelea kuongezeka nchini.
Dk. Ndugulile ameongeza kuwa kwa mujibu wa tafiti, kati ya asilimia 7-15 ya Watanzania wana matatizo sugu ya figo ambayo kwa ukubwa yanasababishwa na magonjwa ya shinikizo la damu na kisukari.
Wafanyakazi wa Dangote wamegoma, RC Mtwara katoa maagizo na maamuzi