Mbunge wa Ileje Aliko Kibona ndio aliuliza swali bungeni akiwa na lengo la kutaka kujibiwa na Wizara ya michezo kuhusu sheria kwamba kila mwajiri ahahakikishe anapomlipa mfanyakazi wake bila kujali aina ya mkataba, anamuwekea pesa katika mifuko ya hifadhi ya jamii.. akijumlishia pia na club za soka Tanzania ziweze kuombwa kuangalia uwezekano kuwekea hifadhi ya jamii wachezaji wake.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Juma Nkamia akawasha vipaza sauti na kusema haya >>> “Tutashirikiana na SSRA kuangalia namna gani sasa tuweze kuzishawishi club zetu ili wachezaji wao waweze kuingia katika mifuko hii.. lakini pia nitumie fursa hii kuipongeza sana klabu ya Yanga kupitia mwenyekiti wake Yusuph Manji.. Yanga tayari wameshazungumza na NSSF na wachezaji wao wote sasa wanapewa mikopo ya nyumba, hii ni hatua moja nzuri na sisi kwa upande wetu tutatumia fursa yetu kuzungumza na club nyingine ili wachezaji wao na waweze kufanya hivyo, hata wale wa Simba…”
Mheshimiwa Ismail Aden Rage alimalizia kwa kujibu hivi; “… Kwa taarifa tu kwa bunge lako tukufu, Simba wanaujenga uwanja wao wa kisasa kule Bunju na watajenga nyumba kwa wachezaji wao…”
Kusikiliza mjadala huo unaweza kubonyeza play hapa chini…
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook