Rais wa Marekani Joe Biden amewasili nchini Israeli kwa ziara ya kuonyesha mshikamano na taifa hilo kufuatia shambulio la kundi la Hamas.
Ziara hiyo pia inakuja wakati huu shambulio kwenye hosipitali moja katika eneo la Gaza ambalo limesababisha vifo vya karibia watu mia tano likizua hofu ya kutokea kwa uhasama zaidi katika eneo hilo la Mashariki ya Kati.
Biden amepokelewa na waziri mkuu Israeli Benjamin Netanyahu wawili hao wakionekana kukumbatiana katika uwanja wa ndege ishara ya mshikamano baina yao.
Mamia ya walinda usalama waliojihami wameonekana katika hoteli seafront mjini Tel Aviv, eneo ambako Netanyahu na Biden wanatarajiwa kuwa na kikao.
Tel Aviv iko kilomita 65 sawa na maili 40 kutoka katika ukanda wa Gaza, makao ya wapiganaji wa Hamas ambao Israeli imekuwa ikiwakabili tangu shambulio la Oktoba 7.
Ziara hii inakuja wakati huu pia kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis akitoa wito wa hatua kuchukuliwa kupesha eneo la Gaza kuinga katika mzozo wa kibinadamu.
Aidha Papa Francis ameonya kuhusu uwezekano wa kupanuka kwa mzozo wa Israeli na Gaza.