Jumamosi ya January 16 mshambuliaji wa Azam FC anayeichezea klabu ya Simba kwa mkopo Joseph Kimwaga aliingia kwenye headlines, baada ya kuandikwa katika gazeti na blog kadhaa kuwa kavunja mkataba na Simba. Kimwaga aliandikwa baada ya kwenda kuonana na viongozi na kutoa dukuduku lake.
Kimwaga aliripotiwa kupishana na baadhi ya maamuzi ya viongozi, hivyo kukosekana kwenye benchi katika mchezo wa Simba dhidi ya Mtibwa Sugar siku ya Jumamosi ya January 16 uwanja wa Taifa Dar Es Salaam, kitu ambacho kilianza kufanya watu waamini ni kweli kavunja mkataba na Simba, Amplifaya ya Clouds FM ilimtafuta ilikujuwa ukweli ni kweli ana tatizo na uongozi, au yameisha.
“Sikuwa na matatizo na viongozi ila nilikuwa na vikwazo au dukuduku moyoni nikaona bora niseme, tatizo ni kuwa mimi niliona kuna vitu vidogo tu vilikuwa haviko sawa, hakuna kitu kizuri kama kuwa mkweli, mimi nilienda nikawaeleza kuwa matatizo yapo, mtu anapofanya jitihada mtendee haki yake apewe acheze, kuna mechi nyingi nilikuwa nakaa benchi moyoni naumia” >>> Kimwaga
Unaweza msikiliza hapa Joseph Kimwaga
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.