Tunae Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo kwenye hii post ambapo kwakuwa leo ni Alhamisi, siku ya TBT inayotumika kukumbuka kumbukumbu za dhahabu, Jokate ametupitisha kwenye picha mbili tatu za wakati akisoma Sekondari enzi hizo na kuzitolea maelezo.
Picha hizi tatu za juu Jokate anasema “Form Four nilipata B-Physics A-Biology A-Chemisrty na kupelekea kuchaguliwa F5 Msalato kusoma mchepuo wa PCB. Nilibadili maamuzi na kusoma Arts- L.H.S. Ilikuwa Big Deal kwangu mtihani wa Mock/Mkoa kushika nafasi ya Pili Kimkoa kwenye Kiingereza na kutokea kwenye Gazeti la shule Smiling face with open mouth and tightly-closed eyes”
“Wengi wa Wanafunzi wenzangu na Marafiki wa O’Level ni medical Doctors, S/O to Dr. Anette Kessy, Dr. Edwin Mutabazi, Dr. Neema Nalitolela, Dr. Judith Boshe!, Dr. Linda August!!! Special Shout Out kwa Mwalimu wetu wa Biology na School Matron Mrs. Adams- alituandaa vizuri. ST 4 Lyf!!!!
Hizi picha mbili hapa juu Jokate amezitolea maelezo yake >>> “TBT Nikiwa Kidato cha Tatu Shule ya Sekondari Mt. Antoni- Mbagala, wanafunzi wenzangu wa Kidato cha Kwanza mpaka Sita walinichagua kuwa kiongozi wao nafasi ya Dada Mkuu Msaidizi, nikawa pia Dada Mkuu baada ya Dada Mkuu kuhama shule. Kwenye picha tukisoma risala kwenye mahafali”
Maelezo ya hizi picha nyingine mbili za juu Jokate anasema “Wanafunzi wa Loyola walinichagua kuwa Dada Mkuu. Nakumbuka nilipokuwa naomba kura wanafunzi walipiga kelele usiongee sana, ushapita. Nilikuwa mdogo mdogo wa umbo na walimu hawakuwa na imani sana namimi kama nitaweza kuongoza shule nzima. Ila wanafunzi wenzangu walinitia moyo”
TBT INTERVIEW YA JOKATE NA MILLARD AYO