Kiungo huyo akizungumza na Athletic kuhusu mada mbalimbali, ikiwa ni pamoja na upinzani kutoka kwa makundi ya LGBT, pamoja na taarifa za kiasi kikubwa cha pesa alichopewa ili kuhamia Mashariki ya Kati.
Henderson alikanusha madai kwamba anapokea pauni 700,00 kwa wiki Al Ettifaq – kwa hakika, anasisitiza pesa ‘hazikutajwa’ wakati wa majadiliano yake na meneja Steven Gerrard kuhusu uhamisho huo.
Nyota huyo wa Uingereza amefichua kuwa alihisi ‘badiliko’ katika klabu ya Liverpool majira ya kiangazi baada ya mazungumzo ya ‘ukweli’ na Jurgen Klopp kuhusu jukumu lake na aliona ni wakati wa kuendelea kucheza soka la kawaida.
Pia alisema shutuma nyingi alizopata, zikiwamo za watu na sababu anazounga mkono, ‘zilimuumiza’ na kusisitiza bado anaunga mkono sababu zile zile na kuziweka karibu na moyo wake na ni kwa sababu hiyo ndiyo maana anaamini kuhamia kwake Saudia kunaweza tu kuwa ‘jambo chanya’.
Akiongea na The Athletic, Henderson alisema: “Naona hilo kama jambo chanya.
“Naona hivyo kwa sababu, kutoka upande wao (Saudi), walijua hilo kabla ya kunisaini kwa hiyo walijua imani yangu ni nini. Walijua ni sababu gani na kampeni ambazo nimefanya huko nyuma na sio mara moja zililetwa.
“Mimi sio mwanasiasa sijawahi kuwa na sikutaka kuwa. Sijawahi kujaribu kubadilisha sheria au kanuni nchini Uingereza, kamwe sijali katika nchi tofauti ambako sitoki. Kwa hivyo sisemi kwamba ninaenda huko kufanya hivyo.
“Lakini ninachosema watu wanajua maadili yangu ni nini na maadili yangu hayabadiliki kwa sababu ninaenda katika nchi tofauti ambapo sheria za nchi zinaweza kuwa tofauti.