Kocha Mourinho alituma barua kwa mkuu wa soka wa UEFA Zvonimir Boban, ambaye ni mwenyekiti wa bodi, akiarifu baraza linalosimamia uamuzi wake baada ya kumuadhibu kwa “lugha ya matusi” aliyoelekeza kwa Anthony Taylor wakati wa fainali ya Ligi ya Europa.
Barua yake ilisomeka hivi: “Katika kukushukuru kwa mwaliko ulionipa kuwa mjumbe wa bodi ya soka ya UEFA, nasikitika kukutaarifu kwamba kuanzia mara sasa siwezi kuonesha ushiriki wangu katika kundi hili.
“In thanking you for the invitation you extended to me to be a member of the UEFA football board, I regret to inform you that, effective immediately, I will be renouncing my participation in this group.
“Masharti ambayo niliamini sana nilipojiunga hayapo tena na nilihisi wajibu wa kuchukua uamuzi huu. Ninakuomba pia uwasilishe uamuzi wangu kwa Rais Bw. Aleksander Ceferin.”
Mourinho alijiunga na bodi hiyo mnamo Aprili tu ilipoanzishwa na Boban na afisa wa zamani Roberto Rosetti.
Haijakamilioka kuwa iwapo uamuzi wa Mourinho unahusiana na marufuku ya muda mrefu aliyopokea Juni 21 baada ya kumshambulia kwa maneno afisa wa mechi, Anthony Taylor, lakini uchaguzi wa maneno katika barua yake unapendekeza hivyo.
Jarida la Sports Brief pia limeripoti kuwa hatua inayofuata ya kocha Mourinho bado haijafahamika baada ya AS Roma kupoteza fainali ya UEFA Europa League dhidi ya Sevilla kwa njia ya kutatanisha.
Mkongwe huyo wa Ureno alijiunga na Waitaliano mwaka 2021 kwa kandarasi ya miaka mitatu, lakini baada ya miaka miwili ya kufanikiwa zaidi na msaada mdogo wa kifedha, kuna shaka ataendelea.
Mourinho aliiongoza Roma kushinda taji la kwanza la UEFA Europa Conference League katika msimu wake wa kwanza akiwa kocha na kufika fainali za kombe la Ulaya mfululizo katika msimu wake wa pili.