Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu kwa kocha wa zamani wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho, February 7 karudi kwenye headlines na kauli mpya baada ya kutokuwa tayari kuzungumzia soka, Jose Mourinho ameamua kuzungumzia soka ikiwa ni wiki sita zimepita toka afukuzwe kazi na Chelsea.
Jose Mourinho ambaye amekuwa akihusishwa kujiunga na Man United ili arithi nafasi ya Louis van Gaal alikuwa hayupo tayari kuzungumzia soka, ila kwa sasa amekubali kulizungumzia hilo na kukiri kuwa yupo karibu kurudi kazini hivi karibuni, licha ya kuwa wengine huwa wanamtafsiri kama jeuri, lakini yeye anasema ni mtu wa kawaida na anajifunza popote.
“Siku zote nimekuwa nikijifunza hata katika sehemu ambayo najihisi ni mtaalam, siku zote mimi sio mkamilifu na nimekuwa nikijifunza kila siku, wakati mwingine katika kazi na hata maisha binafsi, narudi karibuni katika soka sehemu ambayo nahisi ni maisha yangu ya asili” >>> Jose Mourinho
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwapia ungana na MillardAyo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.