Jose Mourinho amekataa mwaliko wa kutafuta suluhu na mpinzani wake wa siku nyingi kocha Roberto Mancini kwa kukataa hadharani mualiko wa chakula cha usiku baada ya mechi ya Chelsea vs Galatasary.
Chelsea wanaikaribisha Galatasary inayofundishwa na Mancini leo kwenye uwanja wa Stamford Bridge katika mchezo wa pili wa raundi ya 16 bora.
Makocha hao wawili wamekuwa wakilumbana mara kwa mara tangu Mourinho alipomrithi Mancini kama ukocha kwenye klabu ya Inter Milan mwaka 2008 hasa baada ya Mancini kujitamba kwamba alichangia kwa kiasi kikubwa katika kuisuka timu ya Milan iliyokuwa ikifundishwa na Mourinho na kuweza kutwaa makombe manne mwaka 2010.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari kabla ya mechi, Mancini alisema angelipia chakula cha usiku na Mourinho ikiwa Galatasary itashinda mechi ya leo lakini wakati Mourinho alipoulizwa kama amekubali mualiko wa Mancini, alitingisha kichwa chake na kusema “hapana”.
‘Kwa sababu sihitaji kufanya jambo baada ya mechi, sifanyi vitu kwa sababu nimeshinda au nimefungwa baada ya mechi kilichopo kichwani ndio nakifanya haijalishi nimeshinda au nimefungwa, sitoweza kwenda kula chakula cha usiku na mtu fulani ambaye ana kazi yangu, na kitu pekee kinachotufananisha ni kwamba wote ni makocha wa timu za soka’
Kama hupendi kupitwa na stori kama hizi, jiweke karibu zaidi na millardayo.com kwa kujiunga na mimi kwenye twitter na instagram kwa jina hilohilo la @millardayo